Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni za sigara haziogopi kusema uongo- Dkt. Ouma

Kampuni za sigara haziogopi kusema uongo- Dkt. Ouma

Je umewahi kujiuliza kwa nini paketi za sigara na bidhaa za tumbaku au matangazo ya bidhaa hizo yana picha na rangi za kuvutia? Shirika la afya ulimwenguni, WHO linasema hiyo ni kampeni ya kampuni za sigara za kuhakikisha kuwa zinaweza rangi na vivutio hata kutumia watu mashuhuri ili kuhakikisha wavutaji wawe wakubwa au wadogo wananasa kwenye mtego wa uvutaji bidhaa hiyo yenye hatari kubwa kwa afya. Sasa leo ikiwa siku ya kutotumia bidhaa za tumbaku, WHO imekuja na maudhui mahsusi ya kuwa na vifungashio visivyo na alama au rangi yoyote na sababu ni nini? Anafafanua hapa Dkt. Ahmed Ouma, mshauri wa  masuala ya tumbaku ofisi ya WHO  kanda ya Afrika alipohojiwa na Assumpta Massoi wa idhaa hii.