#Tanzania: Mwalimu kushindwa kujibu swali alilouliza mwanafunzi kwatia mashaka- Utafiti

#Tanzania: Mwalimu kushindwa kujibu swali alilouliza mwanafunzi kwatia mashaka- Utafiti

Nchini Tanzania hivi karibuni, Benki ya Dunia ilifadhili utafiti juu ya viashiria vya utoaji huduma hususan afya na elimu nchini humo wakati huu ambapo nchi hiyo imeonyesha maendeleo katika sekta ya elimu katika kipindi cha takribani muongo mmoja uliyopita. Mathalani viwango vya kumaliza shule ya msingi viliongezeka kutoka 55% mwaka 2000 hadi 80% mwaka 2012. Hata hivyo matokeo ya utafiti huo yaliyotangazwa hivi karibuni yamebainisha changamoto ambazo zinapaswa kufuatiliwa ili mfumo wa elimu uweze kutoa wanafunzi wanaoweza kuendana na soko siyo tu ndani ya nchi bali pia kimataifa. Je ni mambo yapi hayo? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Dkt. Lucas Katera, Mkurugenzi wa Utafiti, REPOA ambao ndio waliendesha utafiti huo na anaanza kwa kubainisha maeneo ambayo yalihusika.