Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dr wa Hospitali ya Panzi DR Congo ataka ushirikiano zaidi na UM

Dr wa Hospitali ya Panzi DR Congo ataka ushirikiano zaidi na UM

Dr Denis Mukwege, mkuu wa hospitali ya Panzi mjini Bukavu iliyoko Kivu ya Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na kumuelezea nia ya ushirikiano baina ya hospitali yake, Umoja wa mataifa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO kwa ajili ya kunsuru maisha ya maelfu ya wanawake wanaobakwa nchini Congo.

Hospitali ya Panzi Bukavu imejikita katika kuwasaidia wanawake wanaokabiliwa na ukatili na hussani waliobakwa, inawapokea, kuwalisha, kuwatibu, kuwapa ushauri nasaha na kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida. Dr Mukwege anafafanua alichomiomba kwa Ban Ki-moon.

(SAUTI YA DR MUKWEGE)

Dr Mukwege pia amesema ingawa Umoja wa Mataifa una vikosi vingi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini matatizo yanayowakumba wanawake wa nchi hiyo yanahitaji zaidi ya wanajeshi wa kulinda amani.

(SAUTI YA DR MUKWEGE)