Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na mivutano inayoendelea kabla ya uchaguzi DR Congo

Ban asikitishwa na mivutano inayoendelea kabla ya uchaguzi DR Congo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesikitishwa na kutia hofu na taarifa za ongezeko la mivutano ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Mivutano hiyo inaambatana na mazingira ya sintofahamu inayoghubika mchakato wa uchaguzi nchini humo. Ban ametoa wito wa kuheshimu uhuru na haki za msingi kama zilivyoainishwa kwenye katika .

Amezitaka pande zote kujizuia na kueleza misimamo yao kwa njia ya amani ikiwemo katika maandamano yaliyopangwa kufanyika Mei 26.

Pia ametoa wito kwa wadau wote wa siasa DRC kuweka maslahi ya taifa lao mbele kuliko maslahi binafsi na kujihusisha katika mazungumzo yenye lengo la kutatua tofauti zao kwa njia ya amani.

Amewataka kutoa ushirikiano kwa muwezeshaji wa muungano wa Afrika katika majadiliano ya kitaifa .Bwana Edem Kodjo, na kusema Umoja wa Mataifa upo tayari kusaidia juhudi za mwezeshaji huyo.