Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuyapiga jeki mataifa yenye maendeleo duni kunaweza kuiinua dunia:Acharya

Kuyapiga jeki mataifa yenye maendeleo duni kunaweza kuiinua dunia:Acharya

Kuna fursa kubwa katika miaka 20 ijayo ya kubadilisha kabisa dunia., kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa anyehusika nan chi zenye maendeleo duni au LDCs.

Afisa huyo msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Gyan Chandra Acharya ataongoza mkutano wa Umoja wa mataifa wa mataifa yenye maendeleo duni unaoanza Ijumaa hii mjini Antalya, Uturuki.

Mkutano huo utatathimini hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Mwaka 2011 jumuiya ya Kimataifa ilipitisha programu ya utendaji ya Istanbul ambayo ni ya mkakati wa maendeleo endelevu kwa mataifa 48 ya LDCs.

Bwana Acharya anaelezea ni jinsi gami hali ya watu wanaoishi katika mataifa ya LDCs imebadilika tangu kupitishwa kwa programu hiyo

(SAUTI YA ACHARYA)