Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua chombo cha kusaidia kufanikisha SDG namba nne kuhusu elimu

UNESCO yazindua chombo cha kusaidia kufanikisha SDG namba nne kuhusu elimu

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, imezindua chombo cha kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufanikisha lengo la maendeleo endelevu kuhusu elimu, kupitia taasisi yake inayohusika na masuala ya takwimu.

Chombo hicho kitakachokuwa kwenye mtandao wa intaneti kimezinduliwa wakati wa kongamano la 38 la UNESCO mjini Paris.

Taarifa ya UNESCO imesema kuwa takwimu sahihi zinazoweza kuboresha mikakati kuhusu elimu na kuleta matokeo ni muhimu katika kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinapojizatiti kutimiza lengo la maendeleo endelevu kuhusu elimu, SDG 4.

Kupitia taasisi yake ya takwimu, UNESCO inaongoza juhudi za kubuni mikakati na vigezo vinavyohitajika kufuatilia ufanikishaji wa lengo la SDG 4 na malengo madogo husika.