Bibi-mke au nyanya?

Bibi-mke au nyanya?

Katika neno la wiki tunachambua neno bibi, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Maswala ya Mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu Zuberi Bakari anazungumzia matumizi ya neno bibi nchini Kenya na Tanzania.  Anasema Bibi linatumika hutumika Tanzania kwa maana ya mama ya wazazi wa mtu na Kenya, linatumika kwa maana ya mke. Je ni ipi sahihi? Bwana Bakari anasema maana zote zinakubalika.