Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 15 wa jamii ya watu wa asili wahitimishwa

Mkutano wa 15 wa jamii ya watu wa asili wahitimishwa

Hatimaye mkutano wa 15 wa jamii ya watu wa asili umefunga pazia kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani baada ya kudumu kwa majuma mawili. Maudhui ya mkutano yalikuwa utatuzi wa migogoro na amani endelevu ambapo wawakilishi wa jamii asilia kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamejadili mchango wa jamii hizo katika utatuzi wa migogoro na kukuza amani ya jamii. Nini hasa kimejiri wakati wa mijadala mbalimbali? Ungana na Amina Hassan katika ripoti hii.