Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa malazi kwa wakimbizi changamoto kubwa: UNHCR

Ukosefu wa malazi kwa wakimbizi changamoto kubwa: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema ukosefu mkubwa wa fedha kwa ajili ya malazi ya wakimbizi inarudisha nyuma juhudi za kukabiliana na changamoto kubwa duniani ya wakimbizi tangu vita kuu ya pili ya dunia. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA FLORA)

Video yenye hisia za madhila mbalimbali yanayowakumba wakimbizi wakiwamo wa Burundi, Afrika ya kati CAR, Syria na kwingineko,UNHCR imeitoa video hii maalum kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kuhakikisha wakimbizi wanapata malazi.

Mathalani mkimbizi huyu kutoka Burundi anasema

(SAUTI MKIMBIZI)

"Kabla ya kuondoka Burundi niliogopa”

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kimataifa, shirika hilo limesisitiza kwamba juhudi za kutoa malazi toshelevu kwa wakimbizi unakabiliana na upungufu wa dola nusu bilioni na kusisitiza kuwa kampeni hiyo inaitaka sekta binafasi kuchangia malazi kwa wakimbizi milioni mbili.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amenukuliwa akisema malazi ni hitaji la msingi kwa wakimbizi na inabidi yachukuliwe kama haki ya binadamu isiyo na mjadala.