Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafuatilia kwa karibu hali ya kisiasa Brazil: Ban

Nafuatilia kwa karibu hali ya kisiasa Brazil: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema aanafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Brazil.

Ban ametoa wito wa kudumisha utulivu na kuwa na majadiliano miongoni mwa sekta zote za kijamii.

Amesema ana amini kwamba uongozi wa nchi hiyo utazingatia mchakato wa kidemokrasia wa Brazil katika utekelezaji wa utawala wa sheria na katiba.

Katibu Mkuu amesema anashukuru kwa mchango muhimu wa Brazil kwenye kazi za Umoja wa Mataifa.