Skip to main content

Ban awasili Antananarivo Madagagascar

Ban awasili Antananarivo Madagagascar

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akiambatana na mkewe na washirika wake wa karibu, amewasili leo mjini Antananarivo Madagascar na kulakiwa na Rais Hery Rajaonarimampianina na mkewe, waziri wa mambo ya nje wa kisiwa hicho , Beatrice Atallah na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kisiwani humo wakiongozwa na Bi Violet Kakyomya ambaye ni mratibu mkazi wa mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Kwa mualiko maalumu wa taifa Ban akiwemo siku mbili katika mji mkuu Malagas atakuwa na mazungumzo rasmi na Rais siku ya Jumatano yakifuatiwa na mkutano wa pamoja na waandishi habari kwenye ikulu ya taifa hilo.

Pia Ban atapata fursa ya kukutana na Rais wa bunge na seneti na atazindua rasmi ripoti kuhusu “gharama za njaa Madagascar”.

Watu wengine atakaokutana nao ni wadau wa maendeleo nchini humo, sekta binafsi zinazojihusisha na masuala ya kibinadamu, na jumuiya za asasi za kiraia zinazohusika na masuala ya haki za binadamu. Pia Ban na mkewe watazuru miradi mbalimbali ya usaidizi ya Umoja wa mataifa na kuzungumza na wanaonufaika nayo.