Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miondoko ya Jazz yaangaziwa Ikulu ya Marekani

Miondoko ya Jazz yaangaziwa Ikulu ya Marekani

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Jazz yalifanyika Ikulu ya Marekani mwishoni mwa wiki, yakileta nguli wa muziki huo ndani na nje ya nchi.

Mathalani kutoka Afrika Hugh Masekela na hapa Marekani, malkia wa muziki wa taratibu, Aretha Franklin, mcharaza gitaa kutoka Benin, Lionel Loueke, miongoni mwa wachache.

Mwenyeji alikuwa rais Barack Obama kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.