Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Majaribio ya silaha za nyukilia uwe na nguvu:Ban

Mkataba wa Majaribio ya silaha za nyukilia uwe na nguvu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza katika maadhimisho ya miaka 20 ya Kamati ya kuchukua hatua ya nchi wanachama wa Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO.

Katika hotuba yake wakati wa mjadala mjini Vienna, Ban amesema miaka 20 ya CTBTO sio sherehe bali ni ukumbusho wa kazi iliyosalia ya kuhakikisha mkataba huo unakuwa na nguvu ya kisheria.

Amesema miaka 20 iliyopita amewahi kuitumikia kamati hiyo akiwa mwenyekiti ambapo alitumia jina lake ambalo kwa lugha ya Kingereza humaanisha marufuku, kukemea majaribio ya silaha za nyukilia na akayataka mataifa nane ambayo hayajatia saini mkataba kufanya hivyo hima.

Katibu Mkuu amewataka vijana kupaza sauti zao na kuwawajibisha viongozi kwa ajli ya mustakabali mwema wa mataifa yao hususani katika usalama dhidi ya silaha za nyukilia kote duniani.