Dola Milioni 200 kulinda msitu wa Congo

Dola Milioni 200 kulinda msitu wa Congo

Dola Milioni 200 zitatumika katika harakati za kulinda msitu wa Congo ulioko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani.

Hatua hiyo inafutia kutiwa saini kwa makubaliano leo huko Geneva, Uswisi kati ya serikali ya DRC na wadau wa kimataifa, wakilenga kuepusha uharibifu wa msitu huo muhimu zaidi katika kuleta mvua.

Mpango huo ni sehemu ya harakati zinazochochewa mpango wa kuendeleza misitu ya ukanda wa Afrika ya kati, CAFI na ule wa kudhibiti uharibifu wa misitu REDD+ unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Kufuatia hatua hiyo, Priya Gajraj kutoka shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP huko Goma, DRC anasema..

(Sauti ya Priya)

“Ni muhimu pia kwa sababu ni makubaliano ya kwanza yanayoonyesha nia na ambayo yametiwa saini kati ya CAFI na serikali ya nchi iliyo Afrika ya Kati. Na ni mpango mkubwa zaidi kuweza kuhitimishwa na REDD+ barani Afrika, kwa hiyo inatuma ujumbe muhimu.”

Makubaliano mengine ya aina hiyo yalitiwa saini hivi karibuni huko Brazil na Indonesia.