Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muongozo wa kupiga mbizi kuokoa rasilimali za majini na utalii UNEP

Muongozo wa kupiga mbizi kuokoa rasilimali za majini na utalii UNEP

Muongozo wa namna ya kupiga mbizi kunaKOweza kulinda viumbe hai baharini vinavyotishiwa na kukua kwa utalii wa Pwani na kuwezesha ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, unazinduliwa kesho barani Asia kwa kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP na wadau.

Muongozo huo umeandaliwa na sekta binafsi zinazofanya kazi na wapiga mbizi, jamii na serikali .

Kukuwa kwa idadi ya watu wanaopiga mbizi kwa kutumia vifaa maalum vya pumzi huleta watu zaidi katika miamba ya matumbawe ambapo UNEP inasema kuwa kila mwaka wapiga mbizi milioni moja huongezeka hatua inayohatarisha viumbe wa majini na kutoweka kwa watalii.

UNEP imesisistiza kuwa muongozo huo unatarajiwa kutoa ulinzi kwa rasilimali za baharini hasa kwa kuzingatia kwamba unaeleza namna bora ya kupiga mbizi