Skip to main content

Wahamiaji zaidi ya 170,000 waingia Ulaya, na zaidi ya 700 wafa maji:IOM

Wahamiaji zaidi ya 170,000 waingia Ulaya, na zaidi ya 700 wafa maji:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema tangu kuanza kwa mwaka huu IOM wahamiaji na wakimbizi wanaokadiriwa kufikia 177,207 wameingia barani Ulaya kwa njia ya bahari wakiwasili Italia, Ugiriki , Cyprus na Hispania.

IOM inasema kati ya hao watu zaidi ya elfu tano wamewasili siku tatu zilizopita pekee huku watu wengine 375 waliowasili mapema leo kwenye eneo la Messina Italia , wameokolewa baharini wakiwa katika boti zilizoondoka Misri mapema wiki hii.

Kwa wiki hii pekee IOM inasema jumla ya wahamiaji 4100 wameokolewa baharini huko Cicily Italia wakiwa kwenye boti mbalimbali , kutoka Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini tangu usiku wa Jumatatu na watu wengine 9 wamekufa maji baada ya kuzama.