Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunisia yahimizwa ihakikishe uhuru wa wanaopinga utesaji, iwape rasilmali

Tunisia yahimizwa ihakikishe uhuru wa wanaopinga utesaji, iwape rasilmali

Wataalam wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, wametoa wito kwa Tunisia ihakikishe kuwa wanajopo wa mkakati mpya wa kuzuia utesaji wana rasilmali za kutosha na uhuru wa kutekeleza majukumu yao.

Wataalam hao wamesema hayo baada ya kuhitimisha ziara yao ya siku tatu nchini Tunisia hapo jana, Aprili 14.

Wakikaribisha uchaguzi wa wanajopo hilo, wataalam hao wameitaja kama hatua muhimu, lakini wakaongeza kwamba changamoto sasa ni serikali ya Tunisia kuwawezesha kuanza kufanya kazi haraka iwezekanavyo, kwa kuhakikisha wana rasilmali za kutosha.

Aidha, wamesema uhusiano baina ya mashirika mbalimbali ya kibinadamu unapaswa kufafanuliwa ili kuepusha mizozano ambayo huenda ikaathiri ufanisi wa mfumo mzima wa ulinzi na ufuatiliaji wa haki za binadamu nchini humo.