Skip to main content

Ukosefu wa usawa wazidi kukumba watoto Ulaya

Ukosefu wa usawa wazidi kukumba watoto Ulaya

Ukosefu wa usawa unazidi kuongezeka kwenye nchi zilizoendelea, na hivyo kuathiri ustawi wa watoto, limeeleza leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Tathmini hiyo imefanyika kwenye nchi 41 zenye kipato cha juu ikiangazia tofauti kati ya watoto kwenye familia zenye kipato cha kati na watoto kwenye familia maskini zaidi.

Kwa mujibu ripoti hiyo, Denmark inashudhudia kiwango kifupi zaidi cha ukosefu wa usawa kwa ujumla, huku Israel na Uturuki zikishuhudia kiwango kikubwa zaidi, nchi tajiri zaidi kama Canada na Ufaransa zikishuhudia ongezeko kubwa la ukosefu wa usawa.

UNICEF imeongeza kwamba licha ya kupungua katika sekta ya elimu, ukosefu wa usawa umeongezeka katika sekta ya afya kwenye nchi karibu zote zilizotathminiwa.

Miongoni mwa mapendekezo ya UNICEF ni kusaidia familia maskini kupewa kipato zaidi na kuwekeza katika sekta ya elimu na afya kwa kuzingatia usawa baina ya watoto.