Tanzania kutekeleza hatua za kuhimili mabadiliko ya tabianchi hima: Muyungi

Tanzania kutekeleza hatua za kuhimili mabadiliko ya tabianchi hima: Muyungi

Wakati mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi uliofikiwa mjini Paris , COP 21 ukitarajiwa kutiwa saini April 22 jijini New York , bara la Afrika limepitisha kwa kauli moja kuridhiwa kwake kupitia kamati ya wataalamu barani humo.

Katika mahojiano na idhaa hii, Mjumbe wa kamati ya wataalamu wa Afrika wanaowashauri marais kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambaye pia ni msimamizi wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania ,Richard Muyungi amesema nchi yake itatekeleza hima hatua za kuhimili mabadiliko hayo mathalani.

(SAUTI MUYUNGI)

Amesisitiza kuwa mkataba wa COP21 unatoa mwanya kwa nchi zilizoathirika zaidi kufautili ahadi za nchi zilizoendelea hatau inayoweza kusaidia kutimiza malengo.