Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM atoa wito wa uchaguzi wa utulivu Chad

Mwakilishi wa UM atoa wito wa uchaguzi wa utulivu Chad

Akiwa ziarani Chad, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kwa Afrika ya Kati, Abdoulaye Bathily, amewasihi wadau wote wa kisiasa na raia kwa ujumla kujizuia kutumia ghasia wakati wa kuelekea uchaguzi wa rais wa tarehe 10 Aprili nchini humo.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, bwana Bathily amepongeza mshikamano wa wagombea urais, vyama vya kisiasa na raia katika utaratibu wa uchaguzi, akiwasihi wote kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na amani.

Huku akikariri umuhimu kwa serikali kutunza haki ya uhuru wa kujieleza na kuandamana kwa amani, amewasihi wadau wa kisiasa kuendeleza shughuli zao kwa kuheshimu sheria za nchi, na kutatua sintofahamu zao kwa njia halali.

Aidha Bwana Bathily amesisitiza kwamba uchaguzi huru na wazi ni msingi wa kukuza amani na demokrasia nchini Chad.