Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA yatoa mafunzo kwa wataalam kuhusu kutambua Zika haraka

IAEA yatoa mafunzo kwa wataalam kuhusu kutambua Zika haraka

Zaidi ya washiriki 35 kutoka nchi 26 watapewa mafunzo kwenye maabara ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) mwezi huu, kuhusu kutumia mbinu ya teknolojia ya nyuklia katika kugundua virusi vya Zika haraka na kwa uhakika.

Mafunzo hayo ni sehemu ya usaidizi wa IAEA kwa nchi za Amerika ya Kusini na Karibi katika jitihada za kupambana na mlipuko wa Zika, ambazo ni pamoja na kuimarisha uwezo wa nchi hizo kugundua virusi na kudhibiti mbu wanaosambaza virusi hivyo.

Virusi vya Zika husambazwa na mbu aina ya Aedes aegypti walioambukizwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, ugonjwa wa Zika umeenea katika nchi 33 na maeneo mengine ya America tangu kuwepo kwake katika kanda hiyo kulipothibitishwa  mnamo mwaka 2015, na nchi katika kanda nyingine pia zimeathiriwa.