Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya Mawasiliano ya Mtandao Kutumiwa Katika Kuwaelimisha Watu Kuhusu Masuala Mbambali Duniani

Matumizi ya Mawasiliano ya Mtandao Kutumiwa Katika Kuwaelimisha Watu Kuhusu Masuala Mbambali Duniani

Matumizi ya hali ya juu ya mawasiliono ya mitandao yametajwa na Umoja wa Mataifa kama fursa ya kihistoria ya kusaidia na kulinda watu, hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyozinduliwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Ripoti hiyo inaeleza jinsi mitandao ya mawasilino inaweza kuchangia habari kuhusu watu, ukosefu wa ajira , mabadiliko ya bei ya vyakula na masuala mengine ya kiuchumi. Mkurugenzi kwenye masuala kuhusu sera na mipango Robert C. Orr anasema kuwa fursa iliyopo itasaidia katika kukabilina na matatizo yakiwemo tatizo la njaa, umaskini na magonjwa akiongeza kuwa kufanikisha hayo ni lazima hamasisho itolewa hasa kupitia njia za mawasilino ya mtandao.