Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu yazidi kuleta nuru kwa wenye Usonji na familia zao

Elimu yazidi kuleta nuru kwa wenye Usonji na familia zao

Usonji, Usonji, Usonji! Umeendelea kuwa changamoto kubwa kwa wazazi ambao watoto wao wanazaliwa na ugonjwa huo, sambamba na watoto wenyewe.

Usonji ni ugonjwa unaokumba ubongo na kusababisha mtoto au mtu mzima kushindwa kuhusiana na watu wengine na wakati mwingine kushindwa kushiriki ipasavyo katika shughuli za kijamii. Hali hii hufanya baadhi yao kutengwa au kufichwa na familia zao.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa kwa kutambua umuhimu wa watu wenye usonji na nafasi yao katika kuleta maendeleo ya jamii na yao wenyewe, imetenga Aprili pili kuwa siku ya kuelimisha umma kuhusu Usonji na huko Arusha nchini Tanzania wadau wakiwemo Connects Autism Tanzania walihamasisha kufanyika kwa maadhimisho na Assumpta Massoi katika makala hii anatupeleka kwenye viwanja vya makumbusho ya Taifa jijini Arusha.