Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapalestina wawe na uhuru wa kusafiri: OCHA

Wapalestina wawe na uhuru wa kusafiri: OCHA

Leo kukifanyika mashindano ya mbio za marathon mjini Bethlehem kwenye ukingo wa magharibi, kwa ajili ya kuunga mkono haki za wapalestina, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa maeneo ya Palestina yaliyotawaliwa, Robert Piper, amesikitishwa kwamba wanariadha kadhaa kutoka Gaza wamenyimwa haki ya kushiriki mashindano hayo.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA, Bwana Piper amenukuliwa akisema kwamba anafikiria vikwazo vinavyowakumba wapalestina kila siku katika uwezo wao wa kutembelea huru.

Amesema vikwazo hivyo vinawazuia wapalestina kupata huduma za msingi, kutendewa haki, kuwa na miundombinu na kufikia ardhi yao na rasimali zao, na kwa ujumla kuwa na fursa yoyote ya maendeleo.

Akiongeza kwamba hata kama Israel ina haki ya kuchukua harakati ili kukabiliana na changamoto za kiusalama, haipaswi kuchukua hatua ambazo hazina uwiano na changamoto hizo na ambazo zinakandamiza raia wote wa Palestina.