Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yataka ulinzi uwekwe haraka kabla ya watu kuanza kurejea kufuatia makubaliano ya EU na Uturuki

UNHCR yataka ulinzi uwekwe haraka kabla ya watu kuanza kurejea kufuatia makubaliano ya EU na Uturuki

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limezitaka pande zote husika kwenye makubalianio ya karibuni baina ya serikali ya Uturuki na Muungano wa Ulaya EU kuhusu wakimbizi na wahamiaji kuhakikisha ulinzi na usalama unaohitajika kabla ya hatua yoyote ya watu kuanza kurejea.Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua

(TAARIFA YA GRACE)

Hii ni kutokana na pengo kubwa linaloendelea kujitokeza katika nchi zote. UNHCR imesema haipingi kurejea kwa watu bila mahitaji ya ulinzi na wale ambao hawajaomba hifadhi, endapo haki za binadamu zitazingatiwa.

Shirika hilo limesema Ugiriki nchi ambayo imekuwa ikihifadhi maelfu ya watu kwa sababu kwingineko Ulaya wamefunga mipaka yao , mfumo mzima wa kupokea na kushughulikia watu ambao watahitaji ulinzi wa kimataifa ama haufanyi kazi au haupo kabisa kama anavyofafanua msemaji wa UNHCR Melisa Fleming.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

Hakuna anayeshinda njaa au kukabiliwa na baridi hadi kufa, lakini hali haiendani na viwango ambavyo tunadhani lazima viwekwe. Tunatoa onyo hili la umma sasa tukitumai kutakuwa na mabadiliko haraka."