Skip to main content

Ban aipongeza Ukraine kwa mchango wake katika usalama wa Nyuklia

Ban aipongeza Ukraine kwa mchango wake katika usalama wa Nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekutana leo na Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, kandoni mwa mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia unaoendelea mjini Washington D.C. hapa Marekani.

Ban ameipongeza Ukraine kwa mchango wake katika usalama wa kimataifa wa nyuklia.

Kuhusu mzozo unaonedelea Mashariki mwa Ukraine Katibu Mkuu ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama na kusisitiza haja ya haraka ya kutekeleza makubaliano ya Minsk .

Rais Poroshenko kwa upande wake amempa taarifa Ban kuhusu hali ya kisiasa nchini Ukraine.