WHO inawachanja waliokutana na waathirika wa karibuni wa Ebola Guinea

WHO inawachanja waliokutana na waathirika wa karibuni wa Ebola Guinea

Mamia ya watu ambao wanasadikiwa kukutana na watu wanane walioathirika na virusi vya Ebola kwenye miji ya Kusini mwa Guinea ya Nzérékoré na Macenta hivi karibuni, wamepewa chanjo katika jitihada za kukabiliana na mlipuko wa karibuni wa Ebola.

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani WHO Guinea imesema zaidi ya watu 1,000 wamebainika kukutana na waathirika hao kwa njia moja au nyingine na kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Takribani watu 800 wamepatiwa chanjo wiki iliyopita wakiwemo watu 182 wanaochukuliwa kuwa ni hatari kukutana nao. Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)

"Tunafahamu kwamba virusi vinaishi kwa baadhi ya watu hata kwa muda wa mwaka mmoja kwa hiyo ni lazima tuwe tayari ili kuweza kukabiliana na mlipuko."