Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wenye usonji wana uwezo mkubwa kimaarifa

Watu wenye usonji wana uwezo mkubwa kimaarifa

Kuelekea siku ya usonji duniani tarehe Pili Aprili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka hatua za makusudi zichukuliwe kusongesha haki za watu wenye usonji na kuhakikisha wanajumuishwa kwenye jamii ili wachangie maendeleo yao na jamii zao. Taarifa zaidi na Flora Nducha

( TAARIFA YA FLORA)

Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa siku hiyo yenye maudhui Usonji na ajenda 2030 ikiangazia kushirikisha watu wenye hali hiyo ya afya ya ubongo.

(SAUTI BAN)

‘‘Ushirikishwaji na ujumuishwaji wa watu wenye usonji utakuwa muhimu katika kufanikisha jamii jumuishi pamoja inyotarajiwa na malengo ya maendeleo endelevu.’’

Nchini Tanzania shirika la kiraia la Connects Autism linalohamasishs umma kuhusu usonji, limesema mafanikio yanaendelea kupatikana ikiwemo jamii kupeleka watoto wenye usonji shuleni lakini bado kuna changamoto kama asemavyo Mkurugenzi wa shirika hilo Grace Lyimo.

(Sauti ya Grace-1)

Halikadhalika amesema watoto wenye usonji ambalo ni tatizo la kiafya kwenye ubongo, hupata elimu hadi ya msingi pekee hivyo anapendekeza..

(Sauti ya Grace-2)