Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa wito wa uchunguzi wa mapema dhidi ya homa ya Lassa

WHO yatoa wito wa uchunguzi wa mapema dhidi ya homa ya Lassa

Homa ya Lassa imeuwa watu zaidi ya 160 Afrika ya Magharibi, wengi wao wakiwa kutoka Nigeria tangu Novemba 2015 kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Shirika hilo limesema vifo vingi kati ya hivyo vingeweza kuepukwa endapo uchunguzi wa haraka ungekuwepo ili watu hao wapate tiba ya mapema.

Tangu Novemba 2015 Nigeria, Benin, Sierra Leone na Togo vimeripoti visa zaidi ya 300 vya homa ya Lassa na vifo 164. Nigeria ndio yenye visa vingi zaidi vilivyofika 266 huku vifo vikiwa 138 katika majimbo 22 kati ya 34.

Kwa upande wake Benini kumeripotiwa visa 51 na vifo 25 wakati Togo na Sierra leone kila moja imekuwa na visa viwili.

Virusi vya Lassa virusi vinabebwa na panya mwerevu (mastomy rat) anayepatikana Afrika ya Magharibi, na virusi hivyo vinaambukizwa kwa binadamu kwa kugusana,na panya aliyeathirika kwa kumkamata, au kumuandaa kwa chakula au kwa kugusa chakula, au vifaa vya nyumbani vilivyo na kinyesi au mkojo wa panya huyo.