Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi mmoja kati ya 10 atahitaji makazia mapya: UNHCR

Mkimbizi mmoja kati ya 10 atahitaji makazia mapya: UNHCR

Mkimbizi mmoja kati ya wakimbizi 10 wa Syria atahitaji makazi mapya au suluhisho jingine katika miaka mitatu ijayo limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Katika taarifa yake ya kuelezea mkutano wa ngazi ya juu unaofanyika jumatano Machi 30 mwaka huu mjini Geneva na kujadili majaliwa ya wakimbizi wa Syria, UNHCR imesema uhitaji wa kuongeza makazi na mambo mengine yawahusuyo wakimbizi yatajadiliwa.

Taarifa hiyo imefafanua kwamba mkutano huo unafuatia ule wa London uliojikita katika fedha za kukabiliana na changamoto za kibinadamu zitokanazo na wakimbizi milioni 13.5 walioko ndani ya Syria na wengine milioni 4.8 walioko sehemu mbalimbali za ukanda huo.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kuwa wazungumzaji katika mkutano wa hapo kesho ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Mkutano wa jumatano unatangulia ule wa mwezi Spetemba kuhusu wakimbizi utakaofanyika katika ukumbi wa bazara kuu la Umoja wa Mataifa .