Umoja wa Mataifa wakaribisha kuondolewa vikwazo kwa raia walionaswa Syria
Umoja wa Mataifa umekaribisha taarifa kwamba pande zinazohasimiana nchini Syria zimeruhusu raia kutoka na kuruhusu misaada kuwasili katika mji wa kale uitwao Homs.
Mratibu wa ugawaji wa misaada ya dharura katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos amekaribisha hatua hiyo kwa kusema atafuatilia maendeleo ya hatua hiyo ambayo itaruhusu raia kurejea makwao na msaada wa kuokoa maisha ya watu takribani 2,500.
Bi Amos amesema Umoja huo unatarajia vikwazo vinaendelea kuondolewa ili kuruhusu wafanyakazi wa mashirika ya misaada wafikishe misaada hiyo salama kwa mamilioni ya raia waliokwama sehemu mbalimbali nchini humo kufuatia vita vinavyoendelea