Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zao la muhogo sasa kukwamua wakazi wa Rufiji nchini Tanzana- UNCDF

Zao la muhogo sasa kukwamua wakazi wa Rufiji nchini Tanzana- UNCDF

Nchini Tanzania, Umoja wa Mataifa kupitia mfuko wake wa maendeleo ya mitaji, UNCDF unasaidia kukwamua harakati za sekta binafsi na ile ya umma katiak kusongesha maendeleo ya wananchi mashinani. Miongoni mwa harakati hizo ni hatua ya hivi karibuni zaidi ya kusaidia kuinua wakulima wa zao la Muhogo katika wilaya ya Rufiji, mkoa wa Pwani. Wakulima hao wamekuwa wakishuhudia harakati zao za kulima zikigonga mwamba lakini sasa kuna matumaini kwani Umoja wa Mataifa umetia shime, shime ambayo itaongeza kasi ya kutekeleza lengo namba moja la ajenda 2030 la kutokomeza umaskini. Nini kinafanyika? Assumpta Massoi anasimulia zaidi katika makala hii iliyowezeshwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.