Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabia nchi yanashika kasi katika kiwango cha kutisha:Ban

Mabadiliko ya tabia nchi yanashika kasi katika kiwango cha kutisha:Ban

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya mabadiliko ya hali ya hewa, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema viwango vya gesi chafu katika anga vinaendelea kuongezeka na hivyo pia kufanya joto la bahari na nchi kavu kupanda .

Amesema mabadiliko ya tabianchi yanashika kasi katika kiwango cha kutisha. Na fursa ya kupunguza kimataifa kupanda kwa joto kwa nyuzi chini ya 2 Celsius kama zilivyokubaliana serikali duniani kwenye mkutano wa Paris mwezi Disemba mwaka jana ni nyembamba na kasi inashuka.

Amesema athari zake zitamgusa kila mmoja tukishuhudia kuongezeka kwa kiwango cha joto. Mvua na mafuriko kuweka maisha na mali za watu katika hatari huku ukame ukihatarisha usalama wa chakula, kuongeza vifo na kudhoofisha uchumi wa ndani na wa kimataifa. Mabadiliko ya hali ya mazingira yataongeza kuenea kwa magonjwa mengi.

Hivyo wakati kaulimbiu ya Siku ya mwaka huu ya Hali ya Hewa Duniani: "joto la kupindukia, ukame, mvua nyingi: kabiliana na mustakhbali". dunia lazima ichukue hatua sasa ya kubadilisha uchumi wa dunia kwa kupunguza matumizi ya gesi chafu .

Ban amesema amewaalika viongozi wa dunia mwezi ujao, tarehe 22 Aprili, kuja New York kutia saini mkataba uliopitishwa, ambao ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuridhiwa kwake haraka. Pia ametumia siku ya leo kuwaasa viongozi watoa maamuzi na wadau wengine wote katika jamii kukabili mustakhbali wao sasa.Akisema kwa kukabili mabadiliko ya tabia nchi sasa ndio dunia itaweza kuepuka athari kubwa za mabadiliko hayo.