Skip to main content

Leo ni sikuya kimataifa ya misitu, Wananchi watakiwa kuilinda.

Leo ni sikuya kimataifa ya misitu, Wananchi watakiwa kuilinda.

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya misitu, ujumbe wa mwaka huu ukiwa jukumu la misitu katika kusaidia mifumo ya maji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema rasilimali hiyo kote duniani ni muhimu katika kutambua lengo la pamoja kwa ajili ya watu na sayari.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hiyo Ban amesema rasilimali hiyo kote duniani ni muhimu katika kutambua lengo la pamoja kwa ajili ya watu na sayari.

Amesema misitu ni kiungo katika mustakabali wa mafanikio na uendelevu wa hali ya hewa na ndiyo maana malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanataka hatua za mabadiliko za kuilinda.

Nchini Uganda Kamishina wa Wilaya ya Hoima, Isaac Kawooya Araali, amezitolea mwito mamlaka za misitu nchini humo kutekeleza sheria ya upanzi na ihifahdi wa misitu. Katika mahojiano na mwandishi wetu John Kibego pia kiongozi huyo anataja jukumu la wananchi.

(SAUTI ISAAC)