Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misitu ikilindwa tutaokoa fedha: Ban

Misitu ikilindwa tutaokoa fedha: Ban

 

Katika ujumbe wake kwa ajili ya siku ya kimataifa ya misitu,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema rasilimali hiyo kote duniani ni muhimu katika kutambua lengo la pamoja kwa ajili ya watu na sayari.

Ban amesema misitu ni kiungo katika mustakabali wa mafanikio na uendelevu wa  hali ya hewa na ndiyo maana malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanataka hatua za mabadiliko za kuilinda.

Akitolea mfano Katibu Mkuu ameitaja miji inayotegemea misitu kwa maji ya kunywa ikiwamo Bogota, Durban, Jakarta, Madrid, New York,  na Rio de Janeiro na hivyo akasisitiza kuwa ikiwa rasilimali hiyo italindwa na kuhifadhi mabonde ya maji twaweza kuokoa gharama za kujenga miundombinu ya maji.

Ban pia amesema kwa kuzingatia kuwa mwaka mwaka 2025  takribani watu bilioni 1.8 wataishi katika maeneo yenye uhaba wa maji, na kwa kuzingatia ongezeko la watu na uhitaji wa maji, ulinzi wa maji kwa kuongeza misitu ni hitaji la dharura.

Mwaka huu siku ya kimataifa ya misitu inajikita katika jukumu la misitu katika kusaidia mifumo ya maji hasa kwa kuzingatia ni mwaka wa utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, SDGS.