Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laelezea wasiwasi kuhusu mkwamo wa kisiasa Lebanon

Baraza la Usalama laelezea wasiwasi kuhusu mkwamo wa kisiasa Lebanon

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wameeleza wasiwasi wao kuhusu mkwamo wa kisiasa nchini Lebanon, ambapo nchi hiyo imekuwa bila rais kwa zaidi ya miezi 21.

Wajumbe hao ambao walihutubiwa mnamo Jumatano Machi 16 na Mratibu Maalum wa Katibu Mkuu Lebanon, Sigrid Kaag, kuhusu utekelezaji wa azimio lao namba 1701 (2006), wamesema hali hiyo inaathiri kwa kiwango kikubwa uwezo wa Lebanon kushughulikia changamoto zake za kiusalama, kiuchumi, kijamii na kibinadamu.

Aidha, wametoa wito kwa viongozi wote wa Lebanon wazingatie katiba ya nchi yao, na makubaliano ya Taif na Muafaka wa Kitaifa, wa kuweka ustawi na maslahi ya Lebanon mbele ya siasa zao binafsi, na kuwezesha utendaji kazi wa taasisi za kitaifa na utoaji huduma za umma.