Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunatarajia kujadiliana na nchi mbali mbali ili kubadilishana mawazo:Waziri-Kariuki

Tunatarajia kujadiliana na nchi mbali mbali ili kubadilishana mawazo:Waziri-Kariuki

Mkutano wa sitini wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 umeng’oa nanga makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano huo ulianza Machi 14 hna unaendelea adi Machi 24. Kauli mbiu ya mwaka huu imejikita katika kuwawezesha wanawake na uhusiano wake na malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs ambayo yameridhiwa mwaka jana.

Nchi wanachama kupitia wawakilishi wao wanashiriki mkutano ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kubadilishana mawazo ili kuwezesha lengo la usawa wa kijinsia 50 kwa 50 kufikiwa mwaka 2030.

Kutoka Kenya Waziri wa vijana, jinsia na sekta ya umma Cecily Kariuki katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya ameelezea matarajio yake katika mkutano, hapa anaanza kuelezea ujumbe wa Kenya kwa CSW60.