Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo-Addis Ababa

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo-Addis Ababa

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo limefanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuanzia Jumatatu tarehe 13 hadi Alhamis tarehe kumi na sita wiki hii.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja wawakilishi wa kisiasa wa ngazi ya juu, wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wa fedha, masuala ya nje na ushrikiano wa maendeleo, wadau wa kitaasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na wanasekta ya biashara.

Dhamira ya kongamano hilo ilikuwa ni kufikia makubaliano baina ya serikali, ambayo yatakuwa mchango muhimu na kusaidia katika utekelezaji wa ajenda ya maendeleo baada yam waka 2015.

Mwenzetu Priscilla Lecomte amekuwa Addis Ababa, akilifuatilia, na sasa katika Makala hii, anatupasha yaliyojiri katika kongamano hilo.