Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taekwondo kufundishwa kwa wakimbizi kambini : UNHCR

Taekwondo kufundishwa kwa wakimbizi kambini : UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesaini mkataba na Shirikisho la Kimataifa la Taekwondo kwa ajili ya kuwafundisha mchezo huo wakimbizi waliopo Mashariki ya Kati, Asia, Ulaya na Afrika.

Shirikisho la Taekwondo limetoa msaada wa walimu na vifaa kwa miradi ya majaribio iliyopo kwenye kambi za wakimbizi wa Syria Uturuki na Jordan.

Miradi mingine ya kusomesha taekwondo kwa wanaume na wanawake inatarajiwa kuanzishwa Colombia, Ethiopia, Ghana na Ugiriki, huku UNHCR ikisema ni njia ya kuimarisha maisha ya wakimbizi kambini.

Rais wa Shirikisho la Taekwondo ameeleza kwamba taekwondo inaweza kuchezwa popote kwani haihitaji vifaa, wala uwanja, bali mwili wa binadamu pekee.

UNHCR imeongeza kwamba kambi za wakimbizi zinakumbwa na ukosefu wa fursa za kujifunza na kucheza michezo mbalimbali.