Skip to main content

Elimu inahitajika kukomesha ndoa za mapema Sudan Kusini: Ellen Margrethe Loj

Elimu inahitajika kukomesha ndoa za mapema Sudan Kusini: Ellen Margrethe Loj

Siku ya wanawake duniani imeadhimishwa nchini Sudan Kusini ambapo pamoja na mambo  mengine muadhui yaliyotamalaki maadhimisho hayo ni kukomesha ndoa za mapema. Grace Kaneiya na maelezo kamili.

(TAARIFA YA GRACE)

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Sudan Kusini Ellen Margrethe Loj amesisitiza kuwa licha ya kuwa mabadiliko katika utamaduni wa ndoa za mapema hayawezi kutokea kwa usiku mmoja,  muhimu ni.

( SAUTI  LOJ)

"Elimu, elimu, elimu. Nafikiri ni muhimu. Lazima pia tufanyie kazi mila. Ikiwa msichana ataelimishwa, kila mwaka anavyozidi kwenda shule anajiimarisha katika kuandaa mustakabhali wake na watoto wake."

Ametaka jumuiya ya kimataifa hususani katika maeneo ambayo ujumbe wa Umoja wa Mataifa umejikita kuhakikisha masuala ya ukombozi kwa wanawake katika kila nyanja ikiwamo haki zao zinafikiwa.