Skip to main content

Elimu bora iwe daraja la kufikia usawa wa kijinsia : Faraja Nyalandu

Elimu bora iwe daraja la kufikia usawa wa kijinsia : Faraja Nyalandu

Leo ikiwa ni siku ya wanawake duniani, Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini Tanzania, Faraja Nyalandu amesema ili kufikia uwiano wa hamsini kwa hamsini kati ya wanaume na wanawake, lazima wanawake wapewe fursa ya kupata elimu bora.

Amesema hayo akizungumza na idhaa hii, akiongeza kwamba kupitia elimu bora wanawake watapata fursa ya kuwa nguzo ya ustawi na maendeleo na kunufaisha taifa kwa ujumla.

Bi Nyalandu amesema tayari hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuwapatia wanawake nafasi zaidi.

(Sauti ya Bi Nyalandu)

Aidha amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuweka nafasi za upendeleo zilizowekwa kwa ajili ya wanawake katika sekta ya elimu na uongozi akisema

(Sauti ya Bi Nyalandu)