Skip to main content

Hekima kwa wanandoa ni muhimu kuleta amani kwenye kaya: Dkt. Ackson

Hekima kwa wanandoa ni muhimu kuleta amani kwenye kaya: Dkt. Ackson

Tanzania imetajwa kupiga hatua ya kuongeza idadi ya wabunge wanawake katika ripoti ya hivi karibuni ya muungano wa mabunge duniani IPU.

Ripoti hiyo imesema idadi ya wanawake wabunge mwaka 2015 iliongezeka kwa asilimia 0.5 tu , ambayo ni karibu asilimia 23 ya viti vyote vya bunge vilivyopo

Miongoni mwa wabunge wapya ni naibu spika wa Dk Tulia Akson ambaye katika ujumbe wake kwa wanawake nchini Tanzania wakati wa kusanyiko la wanawake kutoka kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG, amewataka kutumia hekima katika kuishi na waume zao ili kukuza amani.

Hata hivyo amesema ndoa nyingi hukumbana na changomoto kutokana na wanandoa kutotambua mazingira tofauti ya makuzi .

( SAUTI DK AKSON)