Mazungumzo ya pande kinzani Syria kurejelewa Machi 9

1 Machi 2016

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura, ametangaza leo kuwa mazungumzo ya amani baina ya pande kinzani za Syria yatarejelewa mnamo tarehe tisa Machi mwaka huu.

Awali, mazungumzo hayo yalikuwa yamepangwa kuanza tena tarehe saba Machi, lakini sasa yamehamishiwa tarehe tisa Machi ili kuruhusu muda zaidi wa kushughulikia masuala ya kivifaa na kiutendaji.

Taarifa kutoka ofisi ya mjumbe huyo imesema kwamba Bwana de Mistura anatazamia kuona washiriki wakimakinika katika mazungumzo hayo, kwa matarajio ya kutekeleza azimio namba 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter