Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Afghanistan na Syria waingia Ugiriki kukimbia Vita:UNHCR

Wakimbizi wa Afghanistan na Syria waingia Ugiriki kukimbia Vita:UNHCR

Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR umebaini kwamba asilimi 94 ya waSyria waliowasili Ugiriki mwezi Januari mwaka huu kwa kupitia safari ya hatari ya baharini wanakimbia vita na machafuko nchini mwao, sawa na asilimia 71 ya Waafghanistan waliohojiwa ambao wamekimbia nchi yao.

UNHCR inatoa takwimu hizo za wakimbizi wa Syria na Afghanistan waliowasili Ugiriki mwezi Januari kama sehemu ya  utafiti unaoendelea  kubaini zaidi kuhusu wakimbizi hawa ni kina nani, wapi wanatoka, kwa nini wanakimbia na nini mahitaji yao ya ulinzi ili serikali ya Ugiriki, UNHCR na washirika wengine waweze kuwasaidia ipasavyo hususani wenye mahitahi muhimu kama wanawake na watoto walio pekee yao.