Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inahofia ongezeko la waomba hifadhi na wakimbizi mipakani na madhila yanayowasibu

UNHCR inahofia ongezeko la waomba hifadhi na wakimbizi mipakani na madhila yanayowasibu

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema linahofia hatua za udhibiti zilizopitishwa hivi karibuni na nchi kadhaa za Ulaya ambazo zinaongeza ugumu kwa wakimbizi na waomba hifadhi barani Ulaya.Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Limesema hatua hizo zinaleta tafrani kwenye vituo vya mipakani na kuongeza shinikizo kwa Ugiriki wakati ikiendelea kusuasua na kukabiliana na kundi kubwa la watu wanaohitaji malazi na huduma muhimu.

Kwa mujibu wa UNHCR tarehe 17 mwezi huu Austria ilitangaza kwamba itaweka idadi ya mwisho kwa siku ya watu kuingia katika mipaka yake kuwa ni 3,200  na waoomba hifadhi 80 tuu wapya ndio watakaosalijiliwa kwa siku. Slovenia nayo ikafuata nyayo ikitangaza hatua kama hizo.

Shirika hilo linasema hatua hizi mpya zinahatarisha ukiukaji wa sheria za Muungano wa Ulaya na kudhoofisha juhudi za kuwa na mtazamo thabiti wa pamoja wa kushughulikia suala la wakimbizi na matatizo ya wahamiaji barani Ulaya.