Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali nne na shule zimeshambuliwa Syria:UM

Hospitali nne na shule zimeshambuliwa Syria:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema takribani hospitali nne na shule moja vimeshambuliwa Jumatatu nchini Syria.

Katika  Idlib eneo la Maarat al-Numan hospitali mbili ikiwemo ya madaktari wasio na mipaka zimeshambuliwa kwa makombora yaliyokatili maisha ya watu tisa na kujeruhi wengine 30.

Hospitali ya taifa ya Maarat al-Numan nayo imeshambuliwa ambako watu watatu wameuawa na wengine sita kujeruhiwa, ilihali watu wengine 13 wamekufa na wengine wengi kujeruhiwa katika kituo cha afyua kinachosaidiwa na Umoja wa Mataifa mjini Azazi.

Ofisi ya haki za binadamu imesema inatiwa hofu na ongezeko la mashambulizi haya dhidi ya vituo vya afya katika mgogoro wa Syria.