Mazungumzo ya amani ya Syria yasitishwa tena

Mazungumzo ya amani ya Syria yasitishwa tena

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura ametangaza leo kwamba ameamua kusitisha kwa muda mazungumzo ya amani ya Syria yaliyokuwa yameanza jumatatu hii.

Amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, akiongeza kwamba amesharatibu awamu nyingine ya mazungumzo ambayo yanatakiwa kuanza tarahe 25 Februari.

Bwana De Mistura ameeleza kwamba upande wa serikali umekuwa na masuala ya kiutaratibu kabla ya kukubali kuangazia masuala ya kibinadamu ambayo yalikuwa yamewekwa kipaumbele na upande wa upinzani. Akisema kwamba hayuko tayari kuongoza mazungumzo bila matokeo ya kuonekana akaeleza zaidi.

(Sauti ya De mistura)

“Umoja wa Mataifa hauwezi kuruhusu masuala ya kiutaratibu yawe muhimu zaidi kuliko matokeo halisi ya hali ya kibinadamu kwa raia wa Syria ambao wanategemea mara hii, tusiwapatie kongamano lakini kitu halisi kwa ajili yao.”