Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila ushirikishwaji, vijana watashawishiwa na makundi ya kigaidi: #Youth2030

Bila ushirikishwaji, vijana watashawishiwa na makundi ya kigaidi: #Youth2030

Mkutano wa kamisheni ya maendeleo ya jamii ya Umoja wa Mataifa ukianza leo New York, Marekani, mwakilishi wa vijana atawasilisha mapendekezo ya kongamano la vijana mbele ya wajumbe mkutano huo wa 54.

Miongoni mwa mapendekezo ni umuhimu wa kushirikisha vijana kwenye uongozi wa serikali, ili wajumuishwe kwenye jamii na wasishawishiwe kujiunga na vikundi venye itikadi kali na katili.

Francine Furaha Muyumbi, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ni rais wa Jumuiya ya vijana wa bara la Afrika, aliyeongoza kikao cha vijana wa Afrika kwenye kongamano hilo ambapo akihojiwa na idhaa hii, amefafanua zaidi.

(Sauti ya Francine)