Skip to main content

Vijana wajiongeze ili kushika fursa za kiuchumi na kisiasa: Francine Muyumba #Youth2030

Vijana wajiongeze ili kushika fursa za kiuchumi na kisiasa: Francine Muyumba #Youth2030

Barani Afrika, vitisho vya kigaidi kutoka vikundi vya waasi kama vile Boko Haram nchini Nigeria au ADF-Nalu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC vimesababishwa na vijana wa maeneo hayo kukataa tamaa na kukosa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Hayo ni maoni ya Francine Furaha Muyumba ambaye ameshiriki Kongamano la vijana lililofanyika wiki hii mjini New York, Marekani na kujumuisha wawakilishi zaidi ya 800 na mawaziri 21 kutoka nchi mbali mbali wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Bi Muyumba, kutoka DRC, ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais wa jumuiya ya vijana wa Afrika tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte, amelezea kipi kifanyike ili kuwezesha vijana kushika nafasi zaidi katika jamii na uongozi. Kwanza ananza kwa kusisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana.