Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rwanda yasahau yaliyopita na kuganga yajayo miaka 16 baada ya mauaji ya kimbari.

Rwanda yasahau yaliyopita na kuganga yajayo miaka 16 baada ya mauaji ya kimbari.

Dunia asilani haiwezi kusahau mauaji ya kinyama na kikatili yaliyotokea Rwanda miaka 16 iliyopita. Lakini nchi hiyo inasema imezingatia msemo yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Inapiga vita ukabila uliokuwa chachu ya mauaji hayo ya kimbari mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya laki nane waliuawa. Ikishirikiana na jumuiya ya kimataifa na hususani Umoja wa Mataifa imehakikisha wahusika wanakabiliana na mkono wa sheria, na haswa kufikishwa katika mahakama ya ICTR inayoshughulikia kesi za mauji hayo ya Rwanda iliyoko Arusha Tanzania.

Lakini je mhakama hiyo imepiga hatua kiasi gani? Imeondoa machungu kwa Wanyarwanda? Na wanaweza kuishi pamoja kwa amani na upendo bila kujali misingi ya kikabila? Ni maswali ambayo majibu yake nimepewa na Aloyce Mutabingwa aliyekuwa mwakilishi wa Rwanda kwenye kesi hizo na sasa ni naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya afrika Mashariki.